FAIDA ZA KUJIUNGA NA VICOBA


FAIDA ZA KUJIUNGA NA VICOBA

1. Kupata fulsa ya mafunzo ya KUJITAMBUA,FEDHA,UJASILIAMALI na UWEKEZAJI na kukuwezesha kushiriki katika shughuli za kiuchumi na uzalishaji mali kwa mtizamo chanya, uelewa na ujuzi mkubwa.

2. Kupata fulsa ya kukutana na watu mbalimbali toka vicoba, serikalini, sekta binafsi, wabia wa vicoba nk katika mafunzo, mikutano, semina, makongamano, uzinduzi na sherehe mbalimbali na kubadilishana ujuzi, mbinu na uzoefu katika shughuli za kifedha, kiuchumi, kijamii na mfumo mzima wa maisha ya kila siku na maendeleo endelevu ndani na nje ya nchi.

3. Kupata fulsa za huduma za fedha kama vile;
    i) kuwa na akiba yako
   ii) kuwa na mfuko wako wa jamii
  iii) kupata mkopo kwa urahisi
  iv) kuwa na bima
   v) kupata mfumo wa malipo kwa urahisi (kielektroniki nk)

4. Kupata fulsa ya kuwa mwalimu wa vicoba na kuwafundisha wengine mfumo wa VICOBA endelevu, kujitambua na kujitegemea, ujasiliamali na fedha.

5. Kupata fulsa ya kupata taarifa za Vicoba, sekta za Fedha na taarifa mbalimbali za maendeleo ya uchumi na za kijamii
Mfano kwa kutumia twitter @VicobaTanzania , Website ; www.vicoba.org

©2015 , Vicoba Benki ya Maendeleo Vijijini

Picture News